Wananchi wapewa tahadhari kuhusu vishoka wa maji
20 November 2024, 2:49 pm
Mara nyingi maunganisho mapya ya maji huwavutia vishoka hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini kwa kuwa BUWSSA haipokei fedha tasrimu kwenye maunganisho mapya ya maji
Na Adelinus Banenwa
Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Bunda BUWSSA wamewataka wananchi kufuata utaratibu kwa maunganisho mapya ya maji ili kuepuka vishoka wanaoweza kuwalaghai
Akizungumza na wakazi wa kata ya Sazira mtaa wa Nyamigunga mkurugenzi wa BUWSSA Bi Esther Giryoma wakati wa zoezi la uzinduzi wa kituo cha kuchotea maji kwa wakazi wa mtaa wa Nyamigunga Sazira amesema mara nyingi maunganisho mapya ya maji huwavutia vishoka hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini kwa kuwa BUWSSA haipokei fedha tasrimu kwenye maunganisho mapya ya maji badala yake fedha zote hulipwa kupitia Control Number,
Diwani wa kata ya Sazira na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Bunda Mhe Michael Kweka ameipongeza BUWSSA kwa kazi nzuri wanayoifanya pia amemshukuru Mhe Rais kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajiri ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri ya mji wa Bunda ikiwema miradi ya maji, elimu , barabara miongoni mwa miradi mingine.
Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa kata ya Sazira mtaa wa Nyamigunga wameshukuru kwa kufikishiwa huduma ya maji safi na salama ambapoawali ilikuwa ni changamoto kwao kutokana na maji kuwa mbali ambapo walikuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu.
Aidha wakazi hao kupitia kwa mtendaji wa mtaa wamehaidi kuilinda miundombinu ya maji ili iweze kuwahudumia wao na vizazi vijavyo.
Vvvvvvvvvvvvvvvvvvv