Mazingira FM

‘Walimu, wazazi shirikianeni kudhibiti utoro kwa wanafunzi’

14 November 2024, 7:52 pm

Diwani wa kata ya Hunyari Mhe Sumera Kiharata akichangia hoja ya utoro wa walimu na wanafunzi shuleni

Ni sahihi kwamba hali ya elimu hairidhishi kutokana na uangalizi na usimamizi mdogo wa wazazi kwa watoto wao.

Na Adelinus Banenwa

Mdhibiti Ubora wa Elimu Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ametoa wito kwa wazazi na walezi kushirikiana na walimu katika kuimarisha nidhamu ya wanafunzi na kudhibiti utoro mashuleni.

Wito huu umetolewa katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025, kilichofanyika leo.

Akiwasilisha hali ya ubora wa elimu, Mdhibiti Ubora wa Elimu Halmashauri ya Wilaya ya Bunda amesema kuwa katika ukaguzi wao, changamoto mbalimbali zimebainika.

Baadhi ya madiwani Bunda DC

Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na utoro wa wanafunzi, ukosefu wa madawati, na tatizo la wanafunzi wa kike kupangishiwa nyumba za kuishi bila usimamizi madhubuti.

Sauti ya mdhibiti ubora wa elimu

Wakichangia taarifa hiyo, baadhi ya madiwani wamesema ni sahihi kwamba hali ya elimu hairidhishi kutokana na uangalizi na usimamizi mdogo wa wazazi kwa watoto wao.

Madiwani hao wamesisitiza kwamba, licha ya juhudi za walimu na serikali, bado kuna changamoto kubwa katika kuhakikisha kuwa elimu inatolewa kwa viwango vinavyokubalika.

Sauti za madiwani kuhusu utoro
George Mbilinyi mkurugenzi Bunda DC

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halamshauri ya wilaya ya Bunda  Ndugu George Stanley Mbilinyi amesema suala la utoro wa wanafunzi shuleni ni kweli upo kwa halmashauri ya wilaya ya bunda ambapo changamoto hiyo inashughulikiwa kwa kushirikiana na watendaji wa vijiji na kata

Pia suala utoro kwa walimu pia amekili upo lakini siyo mkubwa na kwa wale wanaokiuka taratibu hatua za kinidhamu zinachukuliwa dhidi yao.

Sauti ya George Mbilinyi mkurugenzi Bunda DC