Mazingira FM

Wenyeviti waliomaliza muda wao watunukiwa hati za pongezi Bunda stoo

6 November 2024, 9:36 pm

moja ya wenyeviti waliomaliza muda wao wakipokea hati ya pongezi, Picha na Adelinus Banenwa

Viongozi wakemea makundi na usaliti, “mwanachama yeyote atayehusika katika usaliti wa chama na ushahidi ukapatikana adhabu ni moja tu kufukuzwa chama”

Na Adelinus Banenwa

Chama cha mapinduzi kata ya Bunda stoo kwa kushirikiana na diwani wa kata hiyo ndugu Flavian Chacha Nyamageko wametoa hati za pongezi kwa wenyeviti wa mitaa ya kata hiyo waliomaliza muda wao.

katibu wa CCM wilaya ya Bunda Ndugu John Chonya Picha na Adelinus Banenwa

Akizungumza katika hafla hiyo mgeni rasmi ambaye ni katibu wa chama hicho kwa wilaya ya Bunda Ndugu John Chonya amesema chama cha mapinduzi kinapongeza hatua zilizooneshwa na diwani wa kata hiyo pamoja na chama ngazi ya kata kwa kutambua mchango wa viongozi hao wa mitaa ambao wamemaliza muda wao huku akiwapongeza wale walirudi kwenye kinyang’anyiro na kuwatia moyo ambao hawakuteuliwa.

Aidha amesema suala la makundi kwenye chama kwa sasa hayana nafasi kwa kuwa wagombea wote kwa sasa wanasimama kwa tiketi ya chama cha mapinduzi hivyo anaamini makundi yote yaliisha baada ya kura za maoni na uteuzi wa wagombea kwenye chama.

sauti ya katibu wa CCM wilaya ya Bunda Ndugu John Chonya
Katibu wa jumuiya ya wanawake CCM wilaya ya Bunda Ndugu Evodia Zumba Picha na Adelinus Banenwa

Naye katibu wa jumuiya ya wanawake CCM wilaya ya Bunda Ndugu Evodia Zumba amekemea suala la usaliti ndani ya chama huku akitaadharisha kuwa mwanachama yeyote atayehusika katika usaliti wa chama na ushahidi ukapatikana adhabu ni moja tu kufukuzwa chama

Sauti ya wanawake CCM wilaya ya Bunda Ndugu Evodia Zumba

Mjumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa Ndugu Kulwa Kahabi ameelekeza maeneo yote ya wilaya ya Bunda ambayo yanaviashiria vya makundi kuvunja makundi hayo haraka ili chama kinapokwenda kwenye kampeini za uchaguzi basi wawe wanazungumza lugha moja ya kumnadi mgombea wa chama chao.

wajumbe wa mkutano wa kuwatunuku hati za pongezi wenyeviti waliomaliza muda wao Picha na Adelinus Banenwa

Katika hatua nyingine diwani wa kata hiyo Mhe Flavian Chacha Nyamageko amesema wamelazimika kutoa hati hizo za pongezi kwa wenyeviti waliomaliza muda wao kwa kuwa kazi kubwa wamefanya katika kipindi chote cha uongozi wao ndani ya miaka mitano.

sauti ya diwani wa kata hiyo Mhe Flavian Chacha Nyamageko

Kwa upande wao baadhi ya wenyeviti waliopokea hati hizo za pongezi wamekishukuru chama kwa kuona umuhimu wao na kutambua kazi waliyoifanya katika kipindi cha uongozi wao huku wale waliolejea kwenye kinyang’anyiro wakiahidi kumaliza makundi ili kuwa kitu kimoja.

Sauti za Baadhi ya wenyeviti waliopokea hati za pongezi