TCRA yahimiza kutumia mitandao kwa tija
23 October 2024, 10:16 am
Kampeni ya ‘NI RAHISI SANA’ inayofanywa na TCRA inalengo la kuelimisha umma kuhusu fursa zilizopo kwenye mitandao
Na Edward Lucas
Watumiaji wa mitandao wamehimizwa kuitumia kwa tija ili kujipatia kipato na kuepuka matumizi ambayo hayana faida kwao.
Wito huo umetolewa leo na Afisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Kanda ya Ziwa, Benadetha Clement wakati akizungumza na Radio Mazingira Fm katika Kipindi cha Asubuhi leo akielezea kampeni ya ‘NI RAHISI SANA’ inayofanywa na TCRA yenye lengo la kuelimisha umma kuhusu Fursa zilizopo kwenye mitandao na Namna ya kuwa Salama Mtandaoni.
Benadetha amesema TCRA imekuja na mpango huo ili kuonesha jamii fursa zilizopo katika mitandao ambazo zitaisaidia kiuchumi kwa kutangza biashara zao na shughuli zingine ambazo zitawaongezea kipato na kuondokana na wimbo la kukosa ajira
Naye Imelda Salum ambaye ni Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa amesema sehemu nyingine ya kampeni ya hiyo ni kuelimisha na kuisisitiza Namna ya kuwa salama Mtandaoni ambapo watumiaji wa mitandao wamesisitizwa kuchukua hatua mbalimbali zinazoweza kulinda taarifa zao na kuepuka baadhi ya vitendo vitakavyowapelekea katika utapeli wa mitandaoni