Mazingira FM

Nyasana wapata maji ya bomba, BUWSSA yawashukuru kwa ushirikiano

23 October 2024, 9:49 am

Mkurugenzi wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Bunda BUWSSA Bi Esther Giryoma, Picha na Adelinus Banenwa.

Wananchi wa mtaa wa nyasana wameipongeza mamlaka na serikali kwa ujumla kwa kuwakumbuka kuwafikishia huduma ya maji safi kwa kwa wametaabika kwa muda mrefu

Na Adelinus Banenwa

Mkurugenzi wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Bunda BUWSSA Bi Esther Giryoma akabidhi kituo cha kuchotea maji kwa wakazi wa mtaa wa Nyasana kata ya Kabasa halmashauri ya mji wa Bunda.

Mkurugenzi wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Bunda BUWSSA Bi Esther Giryoma, Picha na Adelinus Banenwa

Akizungumza na wakazi hao Bi Esther amesema jukumu la Mamlaka ni kuhakikisha wananchi wote wanapata maji safi na salama

Aidha Bi Esther amewataka wakazi hao kujitahidi kulinda miundombinu ya maji na kukemea wale wote wenye nia ya kuhujumu pia amewasisitiza wakazi hao kulipa ankara za maji pindi wanapochota ili kuufanya mradi huo kuendelea kuwepo.

Sauti ya mkurugenzi wa maji
Baadhi ya wakazi wa Nyasana, Picha na Adelinus Banenwa

Kwa upande wao wananchi wa mtaa wa nyasana wameipongeza mamlaka na serikali kwa ujumla kwa kuwakumbuka kuwafikishia huduma ya maji safi kwa kwa wametaabika kwa muda mrefu kwa kutumia maji ya madimbwi ambayo hutumia na wanyama kama vile ng’ombe na mbuzi.

Sauti ya wakazi wa Nyasana
Mtendaji wa mtaa wa Nyasana Ferister Mbonamengi, Picha na Adelinus Banenwa

Naye mtendaji wa mtaa wa Nyasana Ferister Mbonamengi amesema kutokana na changamoto ya maji iliyokuwa inawakabili wakazi hao walilazimika kukataa ujenzi wa zahanati badala yake walihutaji sana Maji ambapo wamejitolea kuchomba mtaro wenye urefu wa kilometa sita

Bi Mbonamengi amesema bila shaka yoyote watailinda miundombinu hiyo ili iweze kudumu muda mrefu na atahakikisha wananchi wanaotumia maji wanalipa ankara zao kwa wakati.

Sauti ya mtendaji wa mtaa wa Nyasana