DC Naano atoa mkono wa pole familia zilizopoteza ndugu ajali ya Kyandege
27 August 2024, 5:40 pm
Mkuu wa wilaya ya Bunda kwa niaba ya Rais Samia amekabidhi shilingi milioni tano kwa familia zilizopoteza ndugu ajali ya Kyandege Bunda na milion moja na laki nne kwa majeruhi wa ajali hiyo.
Na Naomi Lumbe
Mkuu wa wilaya Bunda Dkt Vicent Anney Naano kwa niaba ya Rais wa jamuhuri ya muunga wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amewakabidhi wafiwa waliopoteza ndugu katika ajali ya Kyandege kiasi cha shilingi million tano.
Dkt Anney, akiwa ameongozana na katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Bunda John Chonya wametembelea familia hizo na kutoa pole hiyo kwa niaba ya Rais kutokana na ajali ya gari iliyotokea kijiji cha kyandege tarehe 25 Agust 2024 kupelekea vifo vya ndugu zao.
Mbali na kiasi hicho kilichotolewa kwa wafiwa pia mkuu huyo wa wilaya amewatembelea majeruhi wa ajali hiyo wanaondelea na matibabu katika hospitali ya Bunda DDH ambapo pia kwa niaba ya Rais amekabidhi kiasi cha shilingi million moja na laki nne 1,400,000 kwa kila majeruhi, ambazo zitawasaidia katika matibabu.
Aidha DC Naano amesema hadi kufikia leo hii takribani watu 9 wamethibitika kupoteza maisha kutokana na ajali
Dkt Baraka James, daktari kutoka hospitali Bunda DDH amesema hospitali hiyo ilipokea majeruhi 15 na watatu kati yao walipatiwa rufaa ya kwenda Bugando kutokana na majeraha walikuwa nayo ambapo walikuwa wamevunjika mifupa akiwemo mtoto mdogo
Dkt Baraka amesema wagonjwa 12 waliendelea kupata matibabu katika hospitali hiyo na baadhi wamesha ruhusiwa kurudi nyumbani.
Nao baadhi ya wanafamilia wamemshukuru Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania dkt Samia Suluhu Hassani kwa kuwa na moyo wa huruma na kuwajali watanzania na kuwagusa hata watu wenye hali ya chini na kumuomba aendelee na moyo wa upendo na huruma.