Project Zawadi yakabidhi jengo lenye nyumba sita za walimu Bunda
23 August 2024, 6:14 pm
Halmashauri ya wilaya ya Bunda ina upungufu wa nyumba 500 za walimu ili kukidhi mahitaji ya walimu.
Na Fadhil Mramba
Halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara inakadiriwa kuwa na upungufu wa nyumba za walimu zaidi ya mia tano ambavyo huwafanya walimu kuishi katika mazingira magumu na hatarishi.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt.vicent Naano wakati akizindua nyumba sita za walimu katika shule ya msingi Busore iliyopo Kijiji cha Bukama kata ya Nyamuswa wilayani Bunda zilizojengwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Project Zawadi ambapo hadi kukamilika kwa mradi huo kimetumika kiasi cha shilingi milioni (176,1920,736) ikiwa kiasi cha shilingi milioni 161,612,736 zimetolewa na shirika la Project Zawadi huku kiasi cha shilingi milioni 14,580,000 ni michango ya wananchi ikijumuisha na uletaji wa via viashiria eneo la mradi.
Ameseme kuwa wilaya inauhitaji wa nyumba za walimu mia nane (800) na zilizopo ni mia tatu 300 hivyo kuwa na upungufu mkubwa wa nyumba za walimu .
Hata hivyo Dkt Naano amelipongeza shirika hilo kwa kuwa msaada mkubwa kwa tarafa ya Chamriho kwa kusaidia miradi mbalimbali na kuwaasa walimu kuzitunza nyumba hizo kwa faida ya baadaye.
Katika hatua nyingine shirika la project zawadi limetoa msaada wa kompyuta mpakato kwa watendaji wawili wa kata za Nyamuswa na Salama ili kusaidia utendaji washughuli mbalimbali za kata zao.