Miaka 30 jela na viboko 6 kwa kosa la ubakaji
30 May 2024, 8:26 pm
Mahakama yamuhukumu mshtakiwa miaka 30 jela kwa ubakaji, miaka 5 kwa kosa la kupoka, kulipa fidia ya milioni moja kwa mtuhumiwa na pia kuchapwa viboko 6.
Na Adelinus Banenwa
Mahakama ya wilaya ya Butiama imemuhukumu kifungo cha miaka 30 jela Mrungu Mahera 23 mkazi wa kijiji cha Mirwa kata ya Mirwa wilayani Butiama kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 14 mwanafunzi wa darasa la 7 shule ya msingi Magunga .
Hukumu hiyo imetolewa na mhe Judith Semkiwa hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Butiama May 29, 2024.
Mbali na adhabu hiyo ya kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kubaka pia mahakama imemuhukumu kifungo cha miaka 5 jela kwa kosa la kumpoka mtoto huyo kabla ya kumbaka.
Aidha mahakama hiyo pia imemuamuru kulipa fidia shilingi milioni moja kwa ajili ya matibabu ya mtoto, pia mshitakiwa huyo achapwe viboko 6.
Awali waendesha mashtaka wa serikali Gastoni Kayombo na Joackimu Butahe wameiambia mahakama kuwa mshatikiwa huyo alitenda kosa la kumbaka mtoto huyo angali akijua ni kinyume cha kifungu cha 130 (1) na (2) (e) na 131 (1) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 malejeo ya mwaka 2022
Pia wamesema alitenda kosa la kumteka mtoto huyo angali akijua ni kinyume na kifungu cha 134 na 35 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 malejeo ya mwaka 2022 hivyo wakaiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa ili liwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo.
Mhe hakimu Judith Semkiwa amesema amelidhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo pa sina kuacha shaka lolote kwamba mtuhumiwa litenda kosa hilo hivyo mahakama inamuhukumu adhabu za kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kubaka, miaka 5 jela kwa kusa la kupoka, kulipa fidia ya shilingi milioni moja kwa muhanga na kupigwa viboko 6.