Mbunge Maboto atoa milion 2 kwa umoja wa bajaji Bunda
4 April 2024, 6:42 pm
Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto ametoa shilingi milioni mbili kwa chama cha waendesha bajaji bunda ikiwa ni sehemu ya kuwaunga mkono katika shughuli zao.
Na Adelinus Banenwa
Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto ametoa shilingi milioni mbili kwa chama cha waendesha bajaji bunda ikiwa ni sehemu ya kuwaunga mkono katika shughuli zao.
Mhe Maboto amekabidhi kiasi hicho cha fedha jana Mara baada ya kukutana na maafisa usafirishaji hao ili kusikiliza kero zao na kuweza kuzitatua.
Mhe maboto amewataka madereva hao kufanya kazi kwa kujituma na kuwa na malengo ili kazi yao iweze kuwasaidia wao na familia zao huku akiwahaidi kuwaunga mkono.
Pia mhe maboto amehaidi kuwachangia kiasi kingine cha shilingi million 2 kabla ya mawakani ili kiweze kutunisha mfuko wao kama chama.
Awali akizungumza mbele ya Mhe mbunge Mwenyekiti wa umoja wa waendesha bajaji Bunda mjini Majula Jackson amesema changamoto kubwa kwa madereva bajaji ni ukosefu wa elimu ya udereva jambo linalipelekea kukosa sifa ya kupata leseni hivyo kujikuta wanagombana na maaskari wa usalama barabarani pindi wapotakiwa kuonesha leseni zao.
Mbali na leseni pia Majula amesema kwa sasa umoja huo una kiasi cha shilingi milioni 4 ambazo zinawasaidia kukopeshana pindi mmoja wao akipata tatizo fedha hizo huwasaidia.