Mazingira FM
Wanaojipitisha kusaka uongozi CCM Bunda waonywa
4 April 2024, 5:42 pm
Katibu awa siasa na uenezi CCM Bunda ndugu Gasper Petro amewaonya wanachama wa CCM wanaopitapita kwa nia ya kugombea nafasi ambazo bado viongozi wake wapo kama vile uwenyekiti, udiwani au ubunge ndani ya wilaya ya Bunda.
Akizungumza katika ziara ya mbunge wa jimbo la Bunda mjini kwenye hafla ya ufunguzi wa shule mpya ya kata ya Bunda mjini ndugu Gasper amesema kama chama hakijatangaza nafasi yoyote hadi leo na chama kinatambua mchango na kazi kubwa wanayoifanya viongozi walioko kwenye nafasi zao.
Amemtaja Mhe mbunge wa jimbo la Bunda mjini Robert Maboto kama profesa wa uchumi ambaye anatumia uwezo wake wa ushawishi bila kelele kuhakikisha miradi mikubwa ya maendeleo inafika Bunda.