Mbunge wa Bunda mjini awataka viongozi wa mitaa na kata kulinda maeneo ya serikali
4 April 2024, 5:24 pm
Mbunge Wa Jimbo La Bunda Mjini Mhe Robert Chacha Maboto amewaomba viongozi ngazi za serikali za mitaa na kata kulinda maeneo ya serikali yaliyotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika maeneo yao.
Na Adelinus Banenwa
Mbunge Wa Jimbo La Bunda Mjini Mhe Robert Chacha Maboto amewaomba viongozi ngazi za serikali za mitaa na kata kulinda maeneo ya serikali yaliyotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika maeneo yao.
Mhe Maboto ameyasema hayo leo katika ziara yake aliyoifanya katika jimbo la bunda mjini kwenye kata za Nyasura na Bunda mjini March 3, 2024.
Katika ziara yake Mhe Maboto ametembelea na kukagua ujenzi wa bweni la watoto wenye mahitaji maalumu shule ya msingi mazoezi , ujenzi wa shule mpya ya azimio zote kutoka kata ya Nyasura lakini pia ameshiriki katika uzinduzi wa shule mpya ya sekondari ya kata ya Bunda mjini.
Mhe maboto amesema kwa sasa serikali ya awamu ya sita inatoa fedha nyingi za miradi lakini changamoto inakuwa maeneo ya kuweka miradi hiyo kama vile shule, vituo vya afya au zahanati.
Katika hafla ya ufunguzi wa shule mpya ya kata ya Bunda mjini Mhe Maboto amesema kwa sasa halmashauri imepokea kiasi cha shilingi million 800 ambazo ni kwa ajili ya ujenzi wa shule lakini fedha hizo hazijatumika kutokana na kukosekana kwa eneo la kujenga shule.