Wananchi Nyasura washiriki kuchimba mitaro wapate maji
8 March 2024, 12:51 pm
Imeelezwa kuwa ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo ni suala muhimu na la msingi katika kujiletea maendeleo katika vijiji na mitaa.
Na Adelinus Banenwa
Imeelezwa kuwa ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo ni suala muhimu na la msingi katika kujiletea maendeleo katika vijiji na mitaa.
Mahali ambapo wananchi hawashiriki wala hawashirikishwi kunakuwa na lawama na mizozo mingi kwa viongozi.
Wananchi wakishiriki husaidia kutambua changamoto na kuweka vipaumbele ili kuibua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuweka mikakati ya utekelezaji katika ngazi ya kijiji/mtaa.
Hayo yameelezwa na Magigi Samweli Kiboko Diwani wa kata ya Nyasura halmashauri ya mji wa Bunda wakati akizungumza na Mazingira fm katika shughuli ya uchimbaji wa mtaro wa kulazimia boma la maji mtaa wa Zanzibar.
Aidha Mtandaji wa Kata ya Nyasura Jenimery Atanas amesema ushiriki na Ushirikishwaji wa wananchi ni fursa ambayo mwananchi anapaswa kuitambua na kuifaidi ili kuleta tija kwenye maisha yake na jamii yake.
Lakini pia kuwawezesha wananchi kujua nafasi yao katika jamii na kutambua ushiriki na ushirikishwaji kama njia ya kuwapatia demokrasia
Naye Mtendaji wa mtaa wa Zanzibar bi. Grace Malicha amesema kuwa ushiriki wa wananchi Kuwawezesha wananchi kumiliki na kujivunia maendeleo yao wenyewe kwa kushirikiana na Serikali na Kuwajengea uwezo na uzoefu katika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo.
Kwa upande wao wananchi walioshiriki shughuli hiyo wamesema Suala la kushiriki na kushirikishwa katika vijiji/mitaa ni la lazima kwa sababu ni haki na wajibu wa kikatiba wa kila mwananchi na kwamba inawawezesha wananchi kuwa na taarifa sahihi na za wakati zinazohusu maisha yao na hivyo kufanya maamuzi sahihi na kuchangia maendeleo ya jamii yao.