Mazingira FM

Butiama: NMB watoa msaada wa million 17 shule ya msingi Madaraka

27 January 2024, 9:13 am

Meneja wa NMB kanda ya ziwa mwenye suti nyeusi akipeana mkono na mkuu wa wilaya ya Butiama.

Mkuu wa wilaya ya Butiama Moses Kaegele amewapongeza bank ya NMB kwa kuwa wadau wa maendeleo katika sekta za elimu na afya na kuendelea kuwa karibu na jamii.

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa wilaya ya BUTIAMA Moses Kaegele amewapongeza bank ya NMB kwa kuwa wadau wa maendeleo katika sekta za elimu na afya na kuendelea kuwa karibu na jamii.

Kaegele ameyasema hayo katika hafla ya kupokea vitanda na magodoro vyenye thamani ya shilingi milioni 17 laki 5 kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum kwa shule ya msingi Madaraka.

Pia amewasisitiza wazazi wenye watoto wenye mahitaji maalumu kuwapeleka shule kwani serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inawajari na inaendelea kuboresha mazingira na miundombinu kwa watoto hao.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo meneja wa NMB kanda ya ziwa Wagofya Mfalamagoha amesema kuwa changamoto za kielimu kwa bank hiyo ni jambo la kipaumbele na nilakuungwa mkono na jamii.

Meneja wa NMB kanda ya ziwa mwenye suti nyeusi akipeana mkono na mkuu wa wilaya ya Butiama.

Aidha amesema kuwa wao kama wadau wanapopata maombi ya kuchangia wanafarijika na wanafanya hivyo ili iwe chachu ya maendeleo katika sekta hiyo muhimu ya elimu.

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Madaraka Deo Mutayomba ameishukuru Bank Ya NMB kwa msaada huo walioupata utasaidia watoto hao wenye mahitaji maalum kukaa shuleni na itaondoa changamoto ya watoto ambao hawawezi kutembea kutokana na hali walizonanzo.