Wanafunzi Esperanto sekondari sasa kusoma kidijitali
17 October 2023, 11:05 am
Shule ya sekondari Esperanto kufungiwa mfumo wa intarnet ili kusaidia ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi shuleni hapo.
Na Avelina Sulus na Taro Michael
Shule ya sekondari Esperanto kufungiwa mfumo wa intanet ili kusaidia ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi shuleni hapo.
Hayo yamesemwa na Mramba Simba Nyamkinda aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 9 ya shule hiyo tangu kuanzishwa mwaka 2012.
Mhe. Mramba ambaye ni diwani wa kata ya Ketare na mkurugenzi wa redio Mazingira Fm amesema mfumo huo wa intarnet utakaofungwa shuleni hapo utasaidia walimu kufundisha hata kama wako nje ya shule hiyo.
Aidha Kupitia risala ya wanafunzi wa kidato cha nne mbele ya mgeni rasmi, Wahitimu hao wamesema walianza masomo yao ya kidato cha kwanza 2020 wakiwa jumla ya wanafunzi 150 ambapo kutokana na changamoto mbalimbali zinazo wakabili wamehitimu wanafunzi 114,huku wanafunzi 36 wakishindwa kuhitimu kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utoro na kuhama.
Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Mwl. Morce Vungu, amesema umbali wa shule na makazi halisi ya wanafunzi imeendelea kuwa tatizo linalowasumbua wanafunzi wa jinsi zote hali inayowapelekea wanafunzi kukatiza masomo yao na wengine kuwa watoro.