DAS Bunda awa mbogo, kuwachukulia hatua watumishi wasiozingatia maelekezo
13 August 2023, 3:26 pm
katibu tawala ameonesha kukerwa na kutoridhika na mahudhurio ya wajumbe katika kikao hicho ambapo kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wakurugenzi iliwataka watendaji wote kutoka kata na 33 na mitaa na vijiji pamoja na maafisa ugani kuwepo katika kikao hicho lakini wengi wao hawakufika.
Na Adelinus Banenwa
Katibu tawala wilaya ya Bunda Mhe Salumu Halfani Mtelela amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri za mji na wilaya ya Bunda kuwachukulia hatua za kinidhamu watendaji wa kata, mitaa na vijiji ambao balozia wa Pamba alifika katika maeneo yao kutoa elimu lakini wao hawakufika katika kikao cha tathmini.
Mhe Mtelela ametoa maagizo hayo leo 12 Augost 2023 katika kikao cha tathmini ya ziara ya balozi wa pamba nchini Aggrey Mwanri iliyoanza tangu tarehe 9 mwezi huu na kutamatika kwa kikao hicho cha tathmini
Katika ujumbe wake katibu tawala ameonesha kukerwa na kutoridhika na mahudhurio ya wajumbe katika kikao hicho ambapo kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wakurugenzi iliwataka watendaji wote kutoka kata na 33 na mitaa na vijiji pamoja na maafisa ugani kuwepo katika kikao hicho lakini wengi wao hawakufika.
Mbali na kuagiza kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu kwa watumishi hao katibu tawala pia amewaagiza watendaji wote wa kata kutoka kata zote 33 za wilaya ya Bunda kufika ofisini kwake siku ya jumatatu saa tatu asubuhi ili kuweza kuzungumza namna ya kusimamaia itifaki za viongozi pindi maelekezo yanapotolewa.
Kikao cha tathmini ya ziara ya Mhe balozi wa pamba Tanzania Aggrey Mwanri kilitanguliwa na taarifa za wakurugenzi kutoka halmashauri zote mbili za wilaya ya Bunda na taarifa kutoka kwa bodi ya pamba kupitia kwa mkaguzi wa zao la pamba wilayani Bunda Hemed Kabea