Namba 116 yasaidia kwa kiasi kikubwa utoaji wa taarifa za ukatili
4 August 2023, 2:33 pm
Lengo la mafunzo haya kati ya vyama vya wenye ulemavu na waandishi wa habari ni kuweka mpango kazi wa pamoja na kuweka mapendekezo wa njia gani zitumike katika kutokomeza ukatili wa kijinsia katika jamii.
Na Adelinus Banenwa
Katika kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana hasa wenye ulemavu shirika la C-SEMA kupitia namba 116 ya huduma kwa mtoto imesaidia kwa kiasi kikubwa utoaji wa taarifa za ukatili katika jamii na wanatarajia kutumia namba hiyo kutuma ujumbe mfupi sms.
Thelma Dhaje meneja huduma ya simu kwa mtoto Tanzania Bara kutoka shirika la C-SEMA amesema kupitia namba hiyo ya 116 kwa siku hupokea simu hadi 1000 za masuala ya ukatili hivyo kama shirika wameona ufanisi upo kupitia namba hiyo.
Mwenyekiti wa chama cha wenye ulemavu wilaya ya Butiama CHIVAWATA ndugu Jeremah Juma Masungu amesema kupitia mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi za umma wilayani Butiama zimekuwa mtari wa mbele katika kutetea haki za wenye ulemavu.
kwa upande wake mkuu wa miradi na mkurugenzi wa huduma ya simu kwa mtoto kutoka shirika la C-SEMA Michael Marwa amesema lengo la mafunzo haya kati ya Vyama vya wenye ulemavu na waandishi wa habari ni kuweka mpango Kazi wa pamoja na kuweka mapendekezo wa njia gani zitumike katika kutokomeza ukatili wa kijinsia katika Jamii.