Mmoja afariki 46 wajeruhiwa ajali ya gari Bunda
5 July 2023, 5:40 pm
Mtu mmoja Anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 amepozea maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali katika eneo la Balili kona Bunda mkoani Mara
Na Adelinus Banenwa
Kijana mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 amepoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali ya basi kampuni ya Johamvia linalofanya safari zake kutokea Kemgesi tarafa ya Ikorongo wilayani Serengeti kwenda Mwanza .
Ajali hiyo imetokea leo July 5, 2023 majira ya asubuhi katika eneo la Balili kona mjini Bunda baada ya dereva kudaiwa kushindwa kupiga kona.
majeruhi wamesema gari hilo licha ya kuwa na mwendo kasi aliyokuwa nao dereva bado gari hilo lilikuwa na changamoto nyingi
Mganga mkuu kutoka hospitali ya Bunda DDH Dkt Pendo Faustine amesema hospitali hiyo imepokea mwili wa kijana mmoja wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 ambaye jina lake halijatambulika pia majeruhi 46 ambapo watano kati yao wamepewa rufaa kwenda Bugando kutokana na hali zao kuwa mbaya na 41 wanaendelea na matibabu hospitalini hapo na hali zao zinaendelea vizuri
Kwa mujibu wa mashuda wa ajali hiyo wameiambia mazingira fm kuwa gari hilo lilikuwa mwendo kasi hivyo baada ya kufika kwenye kona inawezekana bleki ziligoma hivyo kupelekea kumshinda dereva na kupinduka
Kwa upande wao baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wakizungumza na mazingira fm wamesema gari hilo licha ya kuwa na mwendo kasi aliyokuwa nao dereva bado gari hilo lilikuwa na changamoto nyingi kwa kuwa ilipofika mugeta ililazimika kusimama kutokana na gari hilo kutoka moshi mwingi.
Radio Mazingira FM bado inaendelea na jitihada za kumtafurta kamanda wa polisi mkoa wa Mara kufafanua zaidi kuhusu chanzo cha ajali na athari za ajali hiyo.