Baraza la madiwani Bunda mjini lapitisha bajeti ya billion 32, 923,527,000 kwa mwaka wa fedha 2023 na 2024.
10 March 2023, 12:58 pm
Baraza la madiwani halmashauri ya mji wa bunda limeketi katika kikao maalum kujadili rasimu ya mpango wa bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2023-2024.
Kikao hicho cha baraza kimefanyika hii leo tarehe 9 Machi katika ukumbi wa halmasahauri ya mji ambapo waheshimiwa madiwani wamesema hawaridhishwi na mfumo mpya wa mpango wa kuzihudumia kaya masikini TASSAF huku wakibainisha changamoto kuwa ni pamoja na madiwani kutoshirikishwa angali ni wenyeviti wa maendeleo ya kata.
Akijibu hoja za waheshimiwa madiwani katika baraza hilo Kulwa Philemon ambae nimratibu TASSAF halmashauri ya mji wa Bunda amsesema tatizo la upungufu wa vifaa maeneo ya mradi ni kutokana na maelekezo ya TASSAF makao makuu na uwiano uliopo kati ya fedha iliyopo na idadi ya walengwa katika eneo husika.
Aidha amesema kwa muungozo huu kila mtu ambaye ni mlengwa anatakiwa kufanya kazi ndipo atapata fedha ya mradi huo akibainisha kuwa kwa utaratibu uliopo ni kwamba kazi wanatakiwa kufanya walengwa wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 65
Akitamatisha hoja ya TASSAF Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Michael Kweka amesema changamoto kubwa kwenye miradi ndani ya halmashauri ni ushirikishwaji duni wa madiwani ndani ya kata zao.
baraza hilo maalumu limepitisha makadirio ya mapato na matumizi ya bajet ya zaidi ya shilling billion 32, 923, kwa mwaka wa fedha 2023 na 2024.