Mazingira FM

CCM Bunda yakusanya milioni mianne arobaini ujenzi ofisi ya wilaya

5 February 2026, 7:37 pm

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara, Stephen Masato Wasira

Harambee imefanyika ikiambatana na maadhimisho ya miaka 49 ya kuzaliwa kwa chama hicho ambacho ni muungano wa vyama vya Afro shilaz part na chama cha TANU mwaka 1977.

Na Naomi Lumbe

Jumla ya shilingi za kitanzania milioni mianne arobaini (440,000,000) zimepatikana kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya chama cha mapinduzi wilaya ya Bunda kupiti harambee iliyofanyika leo, Februari 5, 2026, katika Chuo Cha Ualimu wilayani Bunda, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara  ndugu. Stephen Masato Wasira.

Katika harambee hiyo, viongozi mbalimbali wa chama kutoka ngazi tofauti, wanachama pamoja na wadau walihudhuria na kuchangia kwa hali na mali. Kupitia harambee hiyo, jumla ya shilingi milioni arobaini (440,000,000) zimepatikana kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya chama cha mapinduzi wilaya ambazo zilichomwa moto kwenye vurugu za baada ya uchaguzi mkuu wa oct 29 mwaka 2025

Akizungumza katika hafla hiyo, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara, Stephen Masato Wasira, amewapongeza wote waliojitokeza kuchangia, akisisitiza mshikamano, umoja na ushirikiano kama nguzo muhimu za kuimarisha chama.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara, Stephen Masato Wasira
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara, Stephen Masato Wasira akipokelewa baada ya kufika kwenye harambee

Aidha, kwa niaba ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bunda, mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bunda Ndugu Abraham Mayaya Magese ametoa shukrani kwa uongozi wa chama taifa, wanachama pamoja na wadau wote kwa mchango wao, akieleza kuwa ujenzi wa ofisi za chama utaimarisha utendaji na huduma za chama wilayani humo.

Harambee imefanyika ikiambatana na maadhimisho ya miaka 49 ya kuzaliwa kwa chama hicho ambacho ni muungano wa vyama vya Afro shilaz part na chama cha TANU mwaka 1977.