Mazingira FM

KARITASI ya Muhoji yawezesha wanafunzi 450 vifaa vya shule

28 January 2026, 10:08 pm

Jumla ya wanafunzi 450 wamepatiwa vifaa vya shule ambavyo ni madaftari na kalamu huku 150 kati yao watashonewa sare za shule kutokana na uwezo wa familia zao.

Na Adelinus Banenwa

Jumla ya wanafunzi 450 kutoka shule ya msingi muhoji wamewezeshwa vifaa vya shule na kanisa katoliki kupita shirika la karitasi ambalo limezinduliwa leo katika parokia hiyo

Akizungumza katika uzinduzi huo Askofu mkuu jimbo kuu Katoliki la Bunda Muhashamu Simon Chibuga Masondole amesema kwa jimbo hilo la Bunda, Parokia ya Muhoji ni parokia ya kwanza kuzindua shirika hilo ambapo malengo yake ni kuhudumia jamii isiyojiweza ikiwemo masikini

Askofu Masondole ametoa wito kwa parokia zingine ndani ya jimbo la Bunda kuiga mfano wa parokia ya Muhoji.

Sauti ya Simon Chibuga Masondole

Kwa upande wake Baba paroko wa parokia ya Muhoji Padri Frank Michael Kasole amesema wazo la kuanzisha shirika la karitasi parokiani hapo ni kutokana na uhitaji wa waumini katika eneo hilo.

baadhi ya wanafunzi waliyopata msaada

Padri Frank amesema kwa siku ya leo jumla ya wanafunzi 450 wamepatiwa vifaa vya shule ambavyo ni madaftari na kalamu huku 150 kati yao watashonewa sare za shule kutokana na uwezo wa familia zao.

Sauti ya Padri Frank Michael Kasole

Baadhi ya wanafunzi kutoka shule ya msingi muhoji wameshukuru kwa msaada walioupata ambapo wamesema utawasaidia huku wakibainisha kuwa wamekuwa wakitumia madaftari madogo lakini kwa sasa wamepata counter book

Sauti ya baadhi ya wanafunzi