Mazingira FM
Mazingira FM
28 January 2026, 9:47 pm

Hofu kwa wanachama wa CCM ilikuwa ni kubwa kutokana na matukio ya vurugu za baada ya uchaguzi lakini kwa sasa viongozi wamejiridhisha kuwa hali ni shwari.
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa wanachama wa chama cha mapinduzi CCM kurejea katika hali yao ya kawaida ikiwemo kuvaa sare za chama na kuondoa makava kwenye pikipiki zao ili kufanya kazi zilizokusudiwa za chama.
Wito huo umetolewa na katibu wa jumuiya ya wazazi chama cha mapinduzi wilaya ya Bunda Ndugu Lucia John Tabuse katika baraza la jumuiya hiyo lililofanyika leo tarehe 28 jan 2026.
Bi Lucia amesema hofu kwa wanachama wa CCM ilikuwa ni kubwa kutokana na matukio ya vurugu za baada ya uchaguzi lakini kwa sasa viongozi wamejiridhisha kuwa hali ni shwari na shughuli za chama zinaendelea kama kawaida.

Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa baraza la wazazi wamesema wamepokea maelekeza kutoka kwenye uongozi wa jumuiya hiyo ngazi ya wilaya ikiwemo kutembelea shule zote za msingi na sekondari ili kuangalia hali ya maudhurio ya wanafunzi shuleni.