Mazingira FM

Mbegu bora mwarobaini wa mabadiliko ya tabia ya nchi kwa wakulima

28 January 2026, 8:47 am

Afisa Kilimo Elton Dickson Mtani akiwa studio za radio mazingira fm ,picha na Catherine Msafiri

Afisa Kilimo Elton Dickson Mtani aeeleza kuwa Mbegu bora zina sifa za kustahimili ukame, magonjwa na wadudu, na zinaweza kukua vizuri hata katika mazingira magumu.

Na Catherine Msafiri,

Wakulima wanakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na mabadiliko ya tabianchi, ikiwemo ukame, mvua zisizotabirika, magonjwa ya mimea na wadudu waharibifu. Hali inayoathiri uzalishaji wa mazao na usalama wa chakula kwa jumla.

Katika kukabiliana na changamoto hizi, Afisa Kilimo Elton Dickson Mtani ameeleza katika mahojiano kwenye kipindi cha uhifadhi na utunzaji wa mazingira kutoka kwenye mradi wa LCSL unaosimamiwa na shirika la Grain to Grow Foundation (GGF) kinachorushwa na radio mazingira FM kuwa matumizi ya mbegu bora ni suluhisho muhimu kwa wakulima.

Mtani amesema Mbegu bora zina sifa za kustahimili ukame, magonjwa na wadudu, na zinaweza kukua vizuri hata katika mazingira magumu.

Sauti ya Afisa Kilimo Elton Dickson Mtani

Aidha amebainisha Kupitia matumizi ya mbegu hizo, wakulima wanaweza kupata kwa Kwenda kununua mbegu kwenye duka la pembejeo au kwa kuandaa mwenyewe.

Zaidi ya hayo,amesema matumizi ya mbegu bora huchangia kuongeza kipato cha mkulima na kuimarisha usalama wa chakula katika jamii.

Sauti ya Afisa Kilimo Elton Dickson Mtani