Mazingira FM

TANAPA Kanda ya Magharibi wapanda miti 7000 birthday ya Rais Samia

27 January 2026, 8:32 pm

Jumla ya miti elfu 7 imepandwa katika hifadhi zote zilizopo kanda ya magharibi

Na Adelinus Banenwa

Wito umetolewa kwa wananchi kupanda miti na kutunza mazingira ili kupunguza athari za mabadiriko ya tabia ya nchi.

Hayo yamesemwa leo Jan 27, 2026 na katibu tawala wilaya ya Bunda Salumu Mtelela wakati wa zoezi la upandaji miti katika eneo la mamlaka ya hifadhi za taifa Tanzania TANAPA kanda ya magharibi lililopo wilayani Bunda mkoani Mara
Mtelela amesema zoezi hili ni kuunga mkono siku ya kuzaliwa ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye pia leo ameadhimisha siku yake kwa kupanda miti.

Sauti ya katibu tawala wilaya ya Bunda Salumu Mtelela

Kwa upande wake afisa muhifadhi mkuu David Kadomo kwa niaba ya Mkuu wa TANAPA kanda ya magharibi amesema zoezi la upandaji miti kwa siku ya leo linalenga kuhifadhi mazingira na kuungana na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika siku yake ya kuzaliwa.

Kadomo amesema kwa siku ya leo jumla ya miti elfu 7 imepandwa katika hifadhi zote zilizopo kanda ya magharibi huku akisema kuna umuhimu mkubwa wa upandaji miti ikiwemo matunda na uhakika wa mvua.

Sauti ya David Kadomo