Mazingira FM

Bibi wa miaka 68 auawa, mtuhumiwa atokomea

26 January 2026, 11:22 am

Picha kwa msaada wa mtandao

“Bibi huyo anashambuliwa mikononi alikuwa amebiba mtoto ndipo mtoto huyo alipochukuliwa na bibi alidondoka huku damu nyingi zikiwa zinamtoka”

Na Adelinus Banenwa

Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Ndabacha Humbikijo Madereke Umri 68 Mkazi Wa  Kijiji Cha Kinyangerere Kata Ya Bugwema halmashauri ya wilaya ya Musoma mkoani Mara amepoteza maisha kwa kukatwa ni kitu chenye ncha kali sehemu ya kichwani na shingoni na mtu asiyejulikana.

Tukio hilo linatajwa kutokea Jan 23, 2026 usiku ambapo inaelezwa mtu asiyefahamika alifika nymbani kwa bibi huyo na kumkata na kitu chenye ncha kali kisha kutokomea kusikojulikana.

Mjumbe wa serikali ya Kijiji cha Kinyangerere kata ya Bugwema Stima Meza, amesema tukio hilo limetokea ambapo hadi sasa bado aliyefanya tukio hilo hajafahamika.

Sauti ya Stima Meza

Mjukuu wa marehemu Bahati Nzumbi  amesema bibi yake alikuwa amekaa nyumbani majira ya usiku yapata saa mbili usiku akiwa na babu yake Pamoja na mkamwana ndipo alitokea mtu na alipoulizwa wewe nani alimshambulia bibi huyo kwa mapanga kisha kutoweka.

Ameongeza kuwa wakati bibi huyo anashambuliwa mikononi alikuwa amebiba mtoto ndipo mtoto huyo alipochukuliwa na bibi alidondoka huku damu nyingi zikiwa zinamtoka sehemu ambazo alizojeruhiwa ambapo ni sehemu ya kichwani shingoni na maeneo ya sikio upande wa kushoto.

Bahati amesema waliwatafuta viongozi ili kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa Kijiji na alipofika alikuta bibi huyo ameshapoteza maisha.

Sauti ya Sauti Bahati Nzumbi

Naye Juma Kabati mwenyekiti wa Kijiji cha Kinyangerere kata ya Bugwema ameiambia Mazingira FM kuwa nikweli tukio hilo limetokea ambapo baada ya kupata taarifa aliwasiliana na jeshi la polisi ambapo taratibu za uchunguzi kubaini nani aliyetekeleza tukio hilo.

Sauti ya Juma Kabati

tunaendelea na jitihada za kutafuta Jeshi la polisi mkoa wa Mara kujua kiini cha tukio hilo.