Mazingira FM

Jengeni utamaduni wa kuwaaga watumishi wanapostaafu

24 January 2026, 7:35 pm

Suala la kuanza kazi ni jambo moja na kumaliza ni jambo lingine hivyo ni vema mtumishi anapofikia hatua ya kustaafu aangwe vizuri.

Na Adelinus Banenwa

Wito umetolewa kwa taasisi za serikali kujenga utamaduni wa kuwaaga vizuri wafanyakazi wao wanapostaafu kutokana na kazi kubwa wanazokuwa wamezifanya katika taasisi hizo.

Hayo yamesemwa  na Salam Khalfan Mtelela katibu tawala wilaya ya Bunda kwenye hafla ya kuwaaga watumishi watatu wa mamlaka ya uhifadhi wa wanyamapori tanzani TAWA.

Katika hotuba yake Mtelela amebainisha kuwa suala la kuanza kazi ni jambo moja na kumaliza ni jambo lingine hivyo ni vema mtumishi anapofikia hatua ya kustaafu aangwe vizuri ili kuutambua mchango wake katika taasisi husika.

Sauti ya Salam Khalfan Mtelela

Kwa niaba ya wastaafu katika hafla hiyo Kamishna Msaidizi mstaafu TAWA Said Ismahil Kabanda amesema ili kukufika katika hatua ya kustaafu vizuri lazima mtumishi wa umma uzingatie mambo kadhaa ambayo ni uadilifu na uaminifu , ushirikiano na umoja, kujituma na kuziishi tunu za shirika.

Sauti ya Kamishna Msaidizi mstaafu TAWA Said Ismahil Kabanda

Katika hafla hii walioagwa ni Kamishna Msaidizi Mstaafu Said Ismahil Kabanda, Kamishna Msaidizi Mstaafu Julias Matiko Wandongo na  Mussa Mugusi Mutani.