Mazingira FM
Mazingira FM
22 January 2026, 5:55 pm

Uwepo wa mfumo huo wa kidigitali umesaidia mambo kadhaa kwa watumishi ikiwemo kupunguza muda wa kufualia maombi ya pensheni.
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa watumishi wa umma walioko kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii ya PSSSF kujiunga na mfumo wa kidigitali wa mfuko huo ili kusaidia kuepuka utapeli
Hayo yamesemwa na kaimu meneja wa mfuko huo mkoa wa Mara ndugu Nuru Mahinya katika semina na waandishi wa habari iliyofanyika kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu namna PSSSF ilivyoboresha huduma zake.
Aidha Mainya amesema uwepo wa mfumo huo wa kidigitali umesaidia mambo kadhaa kwa watumishi ikiwemo kupunguza muda wa kufualia maombi ya pensheni pale mtumishi anapostaafu kwa kuwa saizi mtumishi huyo anaweza kujaza fomu kupitia mtandao.
Pia mfumo huu umesaidia kuepuka utapeli ambao watumishi wamekuwa wakikutana nao hasa wanapostaafu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa MRPC, Jacob Mugini, ameishukuru PSSSF kwa semina hiyo kwa waaandishi wa habari wa mkoani Mara ambapo ameziomba taasisi zingine kutumia waandishi wa habari ili huduma zao wanazozitoa kwa jamii ziweze kufika kiurahisi.
Mwenyekiti huyo wa MRPC ametumia nafasi hiyo pia kuishauri PSSSF kuangalia uwezekano wa kuanzisha tuzo kwa waandishi wa habari nchini wanaofanya vizuri kwenye habari za mfuko huo.