Mazingira FM
Mazingira FM
17 January 2026, 5:11 pm

Hii ikiwa inafikia jumla ya wanafunzi 160 wanaosaidiwa na diwani huyo .
Na Adelinus Banenwa
Wakati serikali ikiwahimiza wazazi na walezi kuhakikisha Watoto wote waliofaulu kufika shuleni hatakama mahitaji wadau mbalimbali wameendelea kusaidia vifaa vya shule kwa baadhi ya Watoto wanaoishi katika mazingira magumu
Mramba Simba Nyamkinda diwani wa kata ya Ketare halmashauri ya wilaya ya Bunda hii leo Jan 17, 2026, ametoa vifaa kwa wanafunzi 12 wa shule ya sekondari ya Esperanto wanaoishi katika mazingira magumu na hii ikiwa inafikia jumla ya wanafunzi 160 wanaosaidiwa na diwani huyo .
Aidha mhe mramba ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwahimiza Watoto wao kuzingatia masomo , na wanafunzi wenyewe kuweka juhudi katika masomo
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi waliopata msaada huo wamemshukuru mhe mramba kwa kuwawezesha kupata vifaa vya shule na kuahidi kusoma kwa bidii ili kutimiza ndoto zao.