Mazingira FM

DC Aswege, wanafunzi wote wapokelewe shuleni bila masharti

14 January 2026, 8:22 am

Hata pale mwanafunzi anapofika shuleni bila sare ya shule, walimu hawapaswi kumzuia bali wanapaswa kumpokea mara moja.

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Mhe. Aswege Enock Kaminyoge, ametoa wito kwa walimu wote wilayani humo kuhakikisha wanawapokea wanafunzi wote wa elimu ya awali, darasa la kwanza pamoja na wanafunzi wa kidato cha kwanza bila kuweka masharti yoyote.

‎Mhe. Aswege ametoa maelekezo hayo leo Januari 13, 2026, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi yake wilayani Bunda.

‎Amesisitiza kuwa hata pale mwanafunzi anapofika shuleni bila sare ya shule, walimu hawapaswi kumzuia bali wanapaswa kumpokea mara moja, huku taratibu nyingine zikifanyika baadaye mwanafunzi akiwa tayari anaendelea na masomo.

Sauti ya Aswege Enock Kaminyoge

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka shule watoto wote wenye umri wa kuanza masomo kabla ya tarehe 31 Januari mwaka huu.

Ameonya kuwa wazazi na walezi watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo watachukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria za nchi.

Sauti ya Aswege Enock Kaminyoge