Mazingira FM

Mtoto wa miaka nane adaiwa kujinyonga Bunda

11 January 2026, 8:44 pm

Tukio hilo limetokea siku ya Jumamosi, Januari 10, 2026, majira ya saa tisa mchana.

Na Adelinus Banenwa

Mtoto aliyetambulika kwa jina la Noel Makumbate Mashauli (8), mkazi wa Mtaa wa Wisegere, Kata ya Sazira, Halmashauri ya Mji wa Bunda, na mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Kilimani, anadaiwa kufariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia tai kwenye mti uliopo nyuma kidogo ya nyumbani kwao.

Kwa mujibu wa wazazi wa mtoto huyo, wameiambia Mazingira FM kuwa tukio hilo lilitokea baada ya mtoto huyo kuachwa nyumbani na ndugu zake wakati wao walipokwenda kutafuta riziki.

Tukio hilo limetokea siku ya Jumamosi, Januari 10, 2026, majira ya saa tisa mchana.

Mariam Charles

Kwa upande wake, Bunuri Masanja, jirani wa familia hiyo, amesema alisikia kelele za kuitwa kabla ya mmoja wa watoto kumfuata kumjulisha tukio hilo. Alipofika eneo la tukio alikuta mtoto huyo tayari amejinyonga, ndipo alipompigia simu mama wa mtoto huyo.

Bunuri Masanja

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Wisegere, Simon Mashauri, amesema baada ya kupata taarifa za tukio hilo alifika eneo la tukio na kuwasiliana na Jeshi la Polisi, ambao walifika na kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya taratibu nyingine za kiuchunguzi.

Mwenyekiti huyo amewataka wazazi na walezi kuwa makini na aina ya picha na video zinazorushwa kupitia televisheni na mitandao ya kijamii, akibainisha kuwa baadhi ya maudhui hayo huonesha vitendo vya vurugu na kujidhuru ambavyo vinaweza kuwachochea watoto kuiga na kusababisha madhara makubwa.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Wisegere, Simon Mashauri,