Mazingira FM
Mazingira FM
2 January 2026, 6:10 pm

Amesema ameona ni vema wakati akifungua mwaka mpya 2026 ashiriki na watoto hao kwa kuwapatia mahitaji mbalimbali kama vile mchele kilo , sukari kilo, juice pamoja na mikate .
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa jamii kuwajali watoto wasiyojiweza na waishio kwenye mazingira magumu ili kuleta faraja kwao.
Wito huo umetolewa na Dr Masinde Bwire Jan mosi 2026 alipofika kituo cha kuhudumia watoto wanoishi mazingira magumu cha Rich Village of Hope kilichopo kijiji cha Nambaza kitongoji cha Dodoma halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara.
Dr Bwire amesema ameona ni vema wakati akifungua mwaka mpya 2026 ashiriki na watoto hao kwa kuwapatia mahitaji mbalimbali kama vile mchele kilo 75, sukari kilo 25, juice pakti 16 pamoja na mikate 100.
Aidha Dr Bwire ameahidi kutoa cherehani 10 ifikapo mwezi June kituoni hapo pia kutoa mashati 80 na majoho 6 ifikapo mwezi march baada ya mahitaji hayo kuombwa kupitia raarifa ya mkuu wa shule inayomilikiwa na kituo hicho na watoto wanaolelewa kituoni hapo.
Daud Benjamin Mkuu wa shule ya sekondari Hope Adventist inayomilikiwa na kituo hicho ameshukuru kwa hatua ya Dr Bwire kufika kituoni hapo na kuwapatia zawadi watoto pia naahadi alizozitoa.

Mwl Benjamin amesema kituo hicho kwa sasa kinawatoto 152 ambao wanapatiwa malezi ya kimwili kiroho na kiakili ikiwemo huduma ya elimu kuanzia darasani la awali mpaka kidato cha nne.
Mwl huyo ametoa wito kwa jamii kuwa na utamaduni wa kujitolea na kuwatembelea watoto walioko kwenye vituo kama hivyo kwa kuwa mahitaji ni mengi na kuondoa fikra kwamba wazungu ndiyo hutoa misaada.
Nao baadhi ya watoto wanaolelewa kituoni hapo wamemshukuru Dr Bwire kwa zawadi alizowapelekea huku waomba wadau wengine kufika kutuoni hapo.