Mazingira FM

Wananchi Mara watahadharishwa mvua zinazonyesha

28 December 2025, 8:31 pm

Mrakibu mwandamizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji Augustine Magere, Kaimu kamanda wa zimamoto na uokoaji mkoa wa Mara

Upande wa madereva Kamanda Magere amesema wasikubali kupita juu ya madaraja  au karvati ambalo limefunikwa na maji kwa kuwa ni ngumu kujua hali ya usalama wa eneo husika , pia ametoa rai kwa wazazi na walezi kuhakikisha watoto hawachezei  kwenye madimbwi au mitaro ili kuepusha changamoto zinazoweza kujitokeza

Na Adelinus Banenwa

Wito umetolewa kwa wananchi kuchukua tahadhari kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo mkoa wa mara

Wito huo umetolewa na Mrakibu mwandamizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji Augustine Magere, Kaimu kamanda wa zimamoto na uokoaji mkoa wa Mara katika mahojiano na radio Mazingira FM ambapo amesema kutokana na taarifa ya mamlaka ya hali ya hewa Tanzania ya kuendea kwa vipindi vya mvua ni vema wananchi kila mmoja kuchukua tahadhari katika eneo alilopo

Akizungumzia upande wa madereva Kamanda Magere amesema wasikubali kupita juu ya madaraja  au karvati ambalo limefunikwa na maji kwa kuwa ni ngumu kujua hali ya usalama wa eneo husika , pia ametoa rai kwa wazazi na walezi kuhakikisha Watoto hawachezei  kwenye madimbwi au mitaro ili kuepusha changamoto zinazoweza kujitokeza

Sauti ya Mrakibu mwandamizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji Augustine Magere, Kaimu kamanda wa zimamoto na uokoaji mkoa wa Mara
Mrakibu mwandamizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji Augustine Magere, Kaimu kamanda wa zimamoto na uokoaji mkoa wa Mara

Katika hatua nyingine Kamanda Magere ametoa tahadhari kwa jamii kuelekea sherehe za mwaka mpya kuhakikisha usalama wa nyumba zao hasa kuepuka kuacha Watoto wamewafungia ndani usiku  pindi wanapokwenda kwenye nyumba za ibada au starehe huku akiwatoa hofu wananchi kuwa jeshi hilo la zimamoto limejipanga vizuri kutoa huduma haraka watakapopata taarifa yoyote ya maokozi kupitia namba 114

Sauti ya Mrakibu mwandamizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji Augustine Magere, Kaimu kamanda wa zimamoto na uokoaji mkoa wa Mara