Mazingira FM
Mazingira FM
24 December 2025, 8:05 pm

Afisa kilimo Elton Dickison Mtani wakulima tumieni mbolea ya samadi ina faida kubwa kwenye kurutubisha udogo mashambani.
Na Catherine Msafiri,
Wakulima wamepewa somo matumizi ya mbolea ya samadi ili kutunza unyevuunyevu kwenye udongo kuepuka athari za mabadiliko ya tabianchi.
Elimu hiyo imetolewa na afisa kilimo Elton Dickison Mtani wakati akizungumza kwenye muendelezo wa vipindi vya mradi wa LCSL vinavyosimamiwa na shirika la Grain to Grow Foundation (GGF)kupitia radio Mazingira fm kuhusu matumizi ya mbolea ya samadi ambapo amebainisha kuwa matumizi ya samadi ya faida mbali mbali ambazo mkulima atazibata kama kuupa udongo rutuba na kutoa mazao mengi.
Aidha amebainisha kuwa zipo changamoto za matumizi ya mbolea ya samadi ambazo wakulima wanakumbana nazo kama ongezeko la magugu shambani
Huku akisisitiza kuwa wakulima wanapaswa kutumia njia nzuri ya kuhifadhi samadi kuepusha kupigwa na jua ama mvua inapunguza rutuba.