Mazingira FM

TRA waja na dawati maalum la uwezeshaji biashara

23 December 2025, 12:08 pm

Ruth Kisinga afisa msaidizi wa kodi TRA akiwa studio za Radio Mazingira FM ,picha na Catherine Msafiri.

Ruth Kisinga afisa msaidizi wa kodi TRA dawati maalumu la uwezeshaji biashara lina umuhimu mkubwa na msaada unatolewa bure kwa wafanyabishara wote nchini.

Na Catherine Msafiri,Wafanyabishara wamekumbushwa kulipa kodi awamu ya nne bila kuchelewa ili kuepuka gharama za faini na walio na changamoto wameaswa kufika kwenye dawati maalumu la uwezeshaji biashara Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA ili kupewa msaada.

Wito huo umetolewa na Ruth Kisinga afisa msaidizi wa kodi TRA alipozungumza kwenye kipindi cha kapu letu kuhusu uwasilishaji wa ritani awamu ya nne na dawati maalumu la uwezeshaji biashara ambapo amesema mfanyabiashara ana haki ya kujisajili TRA na kulipa kodi ili kuleta maendeleo kwa nchi.

Sauti ya Ruth Kisinga afisa msaidizi wa kodi TRA

Aidha akielezea kuhusu dawati maalumu la uwezeshaji biashara amesema lina umuhimu mkubwa na wanatoa misaada bure kwa wafanyabishara wote nchini.

Sauti ya Ruth Kisinga afisa msaidizi wa kodi TRA