Mazingira FM

Milion 330.7 kujenga shule mpya Nyasura

13 December 2025, 8:45 pm

Ujenzi huo utahusisha vyumba vya  madarasa 6, jengo la utawala, vyoo matundu 18, Pamoja na vyumba viwili vya madarasa vya elimu ya awali.

Na Adelinus Banenwa

Kutokana na msongamano wa wanafunzi shule ya msingi Nyasura iliyopo kata ya Nyasura mjini Bunda, Serikali imetangaza mradi wa ujenzi wa shule mpya ya msingi katika kata hiyo lengo likiwa ni kupunguza msongamano wa wanafunzi  katika shule hiyo.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wakati wa kutambulisha mradi huo makamu mkuu wa shule ya sekondari ya Dr Nchimbi Mwal Milembe Nditi amesema tayari kiasi cha fedha shilingi milioni 330.7 kimeshawekwa kwenye akaunti ya shule hiyo.

Nditi ameongeza kuwa ujenzi huo utahusisha vyumba vya  madarasa 6, jengo la utawala, vyoo matundu 18, Pamoja na vyumba viwili vya madarasa vya elimu ya awali.

Sauti ya Mwal Milembe Nditi

Diwani wa kata hiyo Mhe Magigi Samweli Kiboko amesema ujenzi wa shule hiyo utasaidia kwa kiasi kikubwa kujibu changamoto ya msongamano wa wanafunzi katika shule ya msingi Nyasura ambayo ina zaidi ya wanafunzi 1200,  licha ya kujengwa kwa shule mpya ya Azimio mwaka 2023 bado idadi ya wanafunzi Nyasura shule ya msingi iliendelea kuwa kubwa.

Aidha amewataka wananchi kuilinda miundombinu hiyo kwa kuwa inakuja kusaidia changamoto zinazowakabili wao

Sauti ya Diwani wa kata ya Nyasura Mhe Magigi Samweli Kiboko

Nao baadhi ya wakazi wa mtaa wa Nyasura C wameshukuru kwa ujio wa mradi huo kuku wakiahidi kutoa ushirikianao hasa wa ulinzi wa vifaa vya ujenzi ili kusiwepo na ubadhirifu wowote .

Kuhuasu changamoto ya msongamano wa wanafunzi madarasani wamesema uwepo wa shule mpya utasaidia kwa kiasi kikubwa kwa kuwa wakati huu wanafunzi ni wengi hali inayopelekea hata hali ya ujifunzaji kwa wanafunzi kuwa ngumu.

Sauti ya baadhi ya wakazi wa Nyasura