Mazingira FM
Mazingira FM
13 December 2025, 3:11 pm

Afisa lishe mkoa wa Mara Bi.Grace Martine mkoa wa Mara kuna 23.4% ya udumavu kwa Watoto,watoto wakipata vitamini A na dawa za minyoo vifo vya watoto vitapungua kwa 24%
Na Catherine Msafiri ,
Wazazi wameaswa kuhakikisha wanawapeleka watoto wao wenye umri wa miezi 6 hadi miaka 5 kwenye vituo za kutolea huduma za afya ili wawezekupewa matone ya vitamin A pamoja na dawa za minyoo ili kuepuka madhara anayowezakupata mtoto katika ukuaji wake.
Hayo yameelezwa na Afisa lishe mkoa wa Mara Bi.Grace Martine alipozungumza kuhusu umuhimu wa vitamini A na dawa za minyoo kwenye kipindi cha semausikike cha radio Mazingira FM ambapo amesema endapo wazazi watawapeleka Watoto kupata huduma hiyo wataokoa takribani asilimia 24 ya vifo vya Watoto wadogo.
Aidha Bi.Grace akizungumzia hali ya lishe kwa mkoa wa Mara ameeleza kuwa kuna 23.4% ya udumavu kwa Watoto hivyo jamii inapaswa kuishi mtindo bora wa maisha na kuzingatia lishe bora.
Kwa upande wake Afisa lishe halmashauri ya mji wa Bunda Bw.Martine Elias ameeleza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa vitamini A na dawa za minyoo kwa mtoto kwani tafiti zinaonyesha inapunguza vifo vya Watoto wadogo chini ya miaka 5.