Mazingira FM
Mazingira FM
11 December 2025, 5:22 pm

Afisa kilimo Elton Dickson Mtani kilimo mseto ni miongoni mwa mbinu bora zinazoweza kuwasaidia wakulima kukabiliana na changamoto zinazosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.
Na Catherine Msafiri,
Katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi wakulima wameshauriwa kutumia kilimo mseto kama njia moja wapo.
Afisa kilimo Elton Dickson Mtani amesema kuwa kilimo mseto ni miongoni mwa mbinu bora na za kisasa zinazoweza kuwasaidia wakulima kukabiliana na changamoto zinazosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.
Akizungumza katika mahojiano kwenye kipindi cha uhifadhi wa mazingira kupitia radio Mazigira FM Mtani alisema kilimo mseto ambacho kinahusisha kulima mazao zaidi ya aina moja katika shamba moja kama mazao ya chakula ,upandaji wa miti na ufugaji mdogo .
Mtani alifafanua kuwa kuna aina za miti ambayo inashauriwa kupandwa kwenye shamba ili kusaidia kuongeza rutuba Pia aliwataka wakulima kuzingatia kilimo hifadhi.
Mwisho, aliwahimiza wakulima kupata ushauri kutoka kwa maafisa kilimo wa maeneo yao ili kupata mwongozo sahihi wa namna ya kupanga mazao na kutekeleza kilimo mseto kwa ufanisi.