Mazingira FM

Mtoto wa miaka 14 anusurika kubakwa na mzee wa miaka 74

11 December 2025, 12:43 pm

Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wazazi juu ya tabia ya mzee huyo lakini hawakuwa na ushahidi wa kumkamata na ndipo siku ya tukio waliandaa mtego ambao ulipelekea kumnasa mzee huyo akiwa amemfungia mtoto huyo ndani.

Na Adelinus Banenwa

Mtoto mmoja wa miaka 14 jina limehifadhiwa mkazi wa mtaa wa Migungani kata ya Bunda stoo wilayani Bunda mkoani Mara amenusurika kubakwa na mzee wa miaka 74 ambaye pia jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi.

kwa mujibu wa mtoto huyo amesema alimkopesha mzee huyo miwa na siku ya tukio alipita kwake kwenda kumdai pesa ya muwa aliokuwa amemkopesha ndipo mzee huyo alimuita na kumuingiza ndani kisha kufunga mlango kwa ndani hadi pale mwenyekiti alipofika na kuwakuta.

Mtoto muhanga

kwa mujibu wa mashuhuda na majirani wa eneo hilo wanasema imekuwa ni kawaida kwa mzee huyo kuwalaghai watoto wadogo hasa wa shule ya msingi  kwa fedha kidogo kama shilingi 200, 500, 1000, na hadi 2000, kisha kuwabaka.

Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Migungani Alphaxard Waheke ameiambia Mazingira fm kuwa kumekuwa akiletewa malalamiko mengi kutoka kwa wazazi juu ya tabia ya mzee huyo lakini hawakuwa na ushahidi wa kumkamata na ndipo siku ya tukio waliandaa mtego ambao ulipelekea kumnasa mzee huyo akiwa amemfungia mtoto huyo ndani.

Sauti ya Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Migungani Alphaxard Waheke

Mwenyekiti wa mtaa wa Migungani Japhet Marko amesema taarifa za mzee huyo kujihusisha na mapenzi na watoto wadogo amekuwa akizipata kutoka kwa wazazi lakini wazazi hao wamekuwa hawatoi ushirikiano ili kumnasa mzee huyo tofauti na mjumbe wake ambaye amefanikisha mtego wa kumkamata

Japhet ameongeza kuwa amewahi kuzungumza na huyo mzee juu ya tuhuma za vitendo na matukio hayo lakini mzee huyo alikanusha kuhusika.

Sauti ya Mwenyekiti wa mtaa wa Migungani Japhet Marko

Mtendaji wa mtaa wa Migungani Veridiana Felix amesema si mara ya kwanza kupata taarifa za mzee huyo na kilichokuwa kinakwamisha ni ushahidi, na katika tukio la leo amemuhoji binti huyo amesema ni mara ya pili kwenda kwa huyo mzee hali inayoonesha huwenda ni tabia yake kuwarubuni watoto na hatua inayofuata ni kumpeleka polisi ili hatua zaidi za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Sauti ya Mtendaji wa mtaa wa Migungani Veridiana Felix

Hata hivyo mzee huyo amepewa dhamani polisi huku hatua za kiupelelezi zikiwa zinaendelea ili mzee huyo aweze kufikishwa mahakamani hayo ni kwa mujibu wa mtendaji mtaa wa Migungani