Mazingira FM

Watu 2 kati ya 100 Bunda DC wameambukizwa VVU

2 December 2025, 4:24 pm

Mganga mkuu wa halmashauri Bunda Dkt Hamidu Adinani

Wataalamu wa afya wanaendelea kutekeleza afua mbalimbali kwenye jamii ikiwemo kutoa elimu juu ya watu kujikinga na maambukizi mapya ya vvu, kuhamasisha wananchi kupima na kujua afya zao, kuendelea kuhamasisha waliogundulika kuwa na maambukizi kutumia dawa kwa usahihi ili kufubaza virusi hivyo.

Na Adelinus Banenwa

Imeelezwa kuwa 2% ya wakazi wa halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara wanaishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI na wanaendelea kutumia dawa za kufubaza virusi hivyo

Hayo yamesemwa na mganga mkuu wa halmashauri hiyo Dkt Hamidu Adinani wakati akitoa taarifa kwa ngeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI  duniani  DEC 1 ambapo kwa upande wa halmashauri ya wilaya ya Bunda yalifanyika kwenye viwanja vya Kisorya

Dkt Adinani amesema wanaendelea kutekeleza afua mbalimbali kwenye jamii ikiwemo kutoa elimu juu ya watu kujikinga na maambukizi mapya ya vvu, kuhamasisha wananchi kupima na kujua afya zao, kuendelea kuhamasisha waliogundulika kuwa na maambukizi kutumia dawa kwa usahihi ili kufubaza virusi hivyo miongoni mwa afua zingine

Sauti ya Mganga mkuu wa halmashauri Bunda Dkt Hamidu Adinani

Aidha Dkt Adinani amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa huo kwa sababu bado upo na ni hatari na kwa kiasi kikubwa huambukizwa kwa njia ya kujamiiana japo zipo njia zingine.

Mkurugenzi mtendaji wa halamshauri ya wilaya ya Bunda George Stanley Mbilinyi

kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halamshauri ya wilaya ya Bunda George Stanley amesema maadhimisho ya siku ya UKIMWI yanalenga kuwakumbuka wale wote waliopoteza maisha kutokana na janga hilo pia ameihasa jamii kuwalea na kuwapenda watoto wote ambao wazazi wao walifariki kwa ugonjwa wa UKIMWI ili watoto hao wasijione wapweke.

Sauti ya George Stanley Mbilinyi

Mbilinyi amewakumbusha wananchi kuwa kwa halmashauri ya wilaya ina vituo vya kupima zaidi ya 40 hivyo wananchi wavitumie katika kujua afya zao.

Sauti ya George Stanley Mbilinyi