Mazingira FM

Serengeti safari marathon yaunga juhudi utunzaji mazingira

26 November 2025, 2:51 pm

Mkurugenzi wa kampuni ya Tecto Community Company Juma elias Serengeti Safari Marathon yapanda miti katika shule za msingi Balili B ,shule ya msingi Azimio ,Bunda Girls, shule ya ajali ushashi na kunzugu

Na Catherine Msafiri,

Katika kuendeleza juhudi za utunzaji wa Mazingira kuelekea Serengeti Safari Marathon,itakayo fanyika Nov 29 ,2025 Safari Serengeti Marathon  wamepanda miti 2500 leo 26 november.

Mkurugenzi wa Serengeti Safari Marathon Thimoth Mdinka akipanda mti shule ya msingi Balili B

Akizungumza na  radio mazingira Mkurugenzi wa Serengeti Safari Marathon Thimoth Mdinka amesema wamefanya zoezi la upandaji miti katika shule ya msingi Balili B,Kwa niaaba ya shule 5 zilizo gawiwa miti hiyo ikiwa  ni kuendeleza utunzaji mazingira ili kupunguza athari za mabadiriko ya tabia nchi.

Aidha amebainisha kuwa lengo lao nikupanda miti takribani 100,000 kwa mwaka huu 2025

Sauti ya Mkurugenzi wa Serengeti Safari Marathon Thimoth Mdinka
Rahel Bugalu Ndegeye Afisa msaidizi misitu kutoka ofisi ya wakala wa misitu Tanzania (TFS) akizungumza na Mazingira FM

Kwa upande wake Rahel Bugalu Ndegeye Afisa msaidizi misitu kutoka ofisi ya wakala wa misitu Tanzania (TFS) amewashukru wadau kuendelea kujitokeza kuomba miti kwa ajiri ya kupanda ili kutunza mazingira kwani miti hiyo inatolewa bure.

Sauti ya Rahel Bugalu Ndegeye Afisa msaidizi misitu kutoka ofisi ya wakala wa misitu Tanzania

Mratibu wa zoezi hilo ambae ni Mkurugenzi wa kampuni ya Tecto Community Company Juma elias ameeleza miti hiyo 2500 imegawiwa katika shule za msingi Balili B ,shule ya msingi Azimio ,Bunda Girls, shule ya amali ushashi na kunzugu.

Sauti ya Mkurugenzi wa kampuni ya Tecto Community Company Juma elias

Naye Kaimu mkuu  wa kitengo cha maliasili na uhifadhi wa mazingira Halmashauri ya mji wa Bunda Kulwa Masalu Philimoni ametoa wito kwa wakazi wa bunda kuacha kukata miti bila kibali kutoka halmashauri na wapande miti ili kutunza mazingira.

Sauti ya afisa mazingira Kulwa Masalu Philimoni