Mazingira FM
Mazingira FM
24 November 2025, 6:44 pm

Wanaotaka kushiriki Serengeti Safari Marathon walipie mix by yas shilingi 45 kwa mbio za kilometa 5,21 na 42.
Na Catherine Msafiri,
Yas wamesema wataendelea kudhamini shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni Sehemu ya kurudisha shukurani kwa wateja wao.
Hayo yamesemwa na Halid Omary meneja wa yas mkoa wa Mara kwenye uzinduzi wa Serengeti Safari Marathon msimu wa nane ambao umefanyika katika makumbusho ya baba wa Taifa Mwitongo Butiama mkoani Mara lengo likiwa ni kufanya mbio za kiutalii ndani ya hifadhi ya taifa Serengeti.
Omary amewaasa wananchi kutokeza kushiriki mbio hizo kwani ni fursa ya kufanya mazoezi,utalii na utunzaji wa mazingira kwani kila mshiriki atapewa mbegu za asili 20 za miti kwaajiri ya kupanda ili kutunza mazingira.

Aidha amebainisha kuwa mtu anaweza kujisajili kwa kulipia kupitia mix by yas shilingi 45 kwa mbio za kilometa 5,21 na 42

Mkuu wa wilaya ya Butiama Bi.Tecla Mkuchika amezindua rasmi mbio hizo akiwaasa wananchi kulinda amani , ameeleza kuwa mbio za serengeti safari marathon zinafanyika kama hamasa ya utalii kutokana na mbio hizo kufanyika ndani ya hifadhi huku wakihamasisha utunzaji wa mazingira.
Serengeti safari marathon msimu wa nane umezinduliwa leo huku kilele ni tarehe 29 November 2025 ikiwa na kaulimbiu isemayo “Tourism Connect“ ikiwa na maana ya utalii unganishi.