Mazingira FM
Mazingira FM
18 November 2025, 12:54 pm

Rehema Kapile afisa lishe makundi yote sita ya vyakula ni rahisi kupata na hata kwa jamii zenye uchumi wa chini hivyo wajawazito watumie ili kuepukana na athari zinazoweza kutokea akiwa na lishe duni.
Na Catherine Msafiri,
Ukosefu wa lishe bora kwa mama mjamzito yatajwa kunaweza kupelekea mama kupoteza ujauzito au kujifungua mtoto mwenye uzito mdogo ama mtoto njiti
Hayo yameelezwa na Rehema Kapile afisa lishe kutoka Halmshauri ya wilaya ya Bunda wakati akizungumza kwenye kipindi cha kapu letu kutoa elimu kuhusu umuhimu wa lishe kwa mama mjamzito ambapo ameeleza kuwa lishe ni muhimu kwa mama mjamzito kwa faida yake na mtoto

Rehema amebainisha kuwa yapo makundi sita ambayo mama mjamzito anashauriwa kutumia makundi ya vyakula vyenye protini,vyakula vya wanga (carbohydrates),mboga za majani,matunda ,maziwa na bidhaa zake ,vyakula vyenye madini na vitamini ni muhimu kwa mtoto aliyepo tumboni
Aidha Rehema ameeleza kuwa makundi yote hayo ya vyakula ni rahisi kupata na hata kwa jamii zenye uchumi wa chini hivyo wajawazito watumie ili kuepukana na athari zinazoweza kutokea kama za kupoteza mtoto ,kujifungua mtoto mwenye uzito mdogo au mama kupoteza maisha
Aidha kwa upande wake mratibu wa elimu ya afya kwa umma kutoka Halmashauri ya wilaya ya Bunda Bi.Magreth Arbogast amesema wanatoa elimu ya lishe kwa jamii ili kuwawezesha wajawazito kuwa na lishe bora wakati wa ujauzito mpaka anapojifungua.
Hata hivyo wameeleza vitu ambavyo mama mjamzito hapaswi kutumia wakati wa ujauzito.