Mazingira FM
Mazingira FM
14 November 2025, 7:04 pm

Katika ujumbe wake kwenye ufunguzi wa maonesho hayo ya siku tatu ameelekeza mambo manne kwa wadau, mambo hayo ni pamoja na wadau wa kilimo misitu washirikiane na serikali ili kutekeleza mikakati ya kitaifa na kimataifa hasa mkakati wa kilimo misitu.
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa wadau wa kilimo kushirikiana na serikali kuwa na kilimo bora na chenye tija ambacho kinaakisi changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi.
Hayo yamesemwa na Yasinta Nzogera, Mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya mazao kutoka wizara ya kilimo katika maonesho ya 10 ya kilimo misitu yanayofanyika katika kituo cha mafunzo cha Vi Agroforestry Bweri Musoma.
Katika ujumbe wake kwenye ufunguzi wa maonesho hayo ya siku tatu ameelekeza mambo manne kwa wadau, mambo hayo ni pamoja na wadau wa kilimo misitu washirikiane na serikali ili kutekeleza mikakati ya kitaifa na kimataifa hasa mkakati wa kilimo misitu. Pili wadau wote wa kilimo misitu na mazingira kufanya kazi kwa karibu na kamati ya kitaifa ya ushauri ya kilimo misitu. Tatu kuanzishwa kwa jukwaa la kilimo misitu lakitaifa litakaloratibu utekelezaji wa mkakati huo pamoja na kuunganisha juhudi na wadau mbalimbali na nne wadau wa kilimo misitu wahakikishe kuwa utekelezaji wa mikakati na shughuli zote unachangia moja kwa moja katika kuimarisha usalama wa chakula nchini

Kwa upande wake Stella Msami afisa ufuatiliaji na tathmini kutoka shirika la Vi Agroforestry amesema katika kipindi cha miaka 40 ya shirika hilo wametekeleza kwa vitendo falsafa yao ya kilimo misitu ambapo wamepanda zaidi ya miti milioni 150 kutoa elimu kwa jamii na mashirika na halmashauri za wilaya na miji katika kukabiliana na mabadiriko ya tabia ya nchi.
Msami amesema katika utelezaji huo pia wanashirikiana na wataalamu mbalimbali kutoka Afrika Mashariki SIAN ambao wanatumika katika utengenezaji wa sera na ushauri kwa wakulima na katika kutekeleza program za Vi Agroforestry ikiwemo ile ya Asili B cc .