Mazingira FM

Bunda DC inavyoshiriki kutoa elimu ya kilimo misitu

14 November 2025, 6:53 pm

Elimu inaendelea kutolewa kwa wakulima kupitia vikundi na wanatoa uwezeshaji hasa kwa vikundi, vya vijana ,akinamama pamoja na wenye ulemavu kupitia fedha za asilimia kumi mapato ya halmashauri.

Na Adelinus Banenwa

Afisa kilimo halmashauri ya wilaya ya Bunda Ndugu Johanes Bucha amesema halmashauri hiyo inashirikiana na wakulima kutekeleza Afua mbalimbali za kilimo misitu na program ya kukabiliana na athari mabadiliko ya tabia ya nchi.

Bucha ameyasema hayo katika maonesho ya 10 ya kilimo misitu yanayofanyika viwanja vya Vi Agroforestry Bweri Musoma ambapo pamoja na mambo mengine maonesho hayo yanatumika katika kutoa elimu kwa wadau wa kilimo na mazingira ili kupata tija kupitia kilimo na kulinda mazingira

Akiwa ameambatana na wakulima na wanufaika wa elimu ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi Bucha amesema elimu inaendelea kutolewa kwa wakulima kupitia vikundi na wanatoa uwezeshaji hasa kwa vikundi, vya vijana ,akinamama pamoja na wenye ulemavu kupitia fedha za asilimia kumi mapato ya halmashauri.

Wakizungumza katika maonesho hayo baadhi ya wakulima walioleta bidhaa zao kutoka halmashauri ya wilaya ya Bunda kutoka vijiji vya Nampindi na Karukekere wamesema mbali na msaada wa kitaalamu wanaoupata kutoka halmashauri pia wamepata uwezeshwaji wa kufedha kwa kupata mikopo isiyo na riba.

Miongoni mwa wakulima hao ni pamoja na wakulima wa Alizeti kutoka Karukekere, wauzaji wa miti ya matunda vivuli na ambao kutoka Nampindi n.k

Afisa kilimo halmashauri ya wilaya ya Bunda Ndugu Johanes Bucha
Aliyeshika mic Yasinta Nzogera, Mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya mazao kutoka wizara ya kilimo

Katika ujumbe wake katika maonesho hayo Yasinta Nzogera, Mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya mazao kutoka wizara ya kilimo ameelekeza mambo manne kwa wadau, mambo hayo ni pamoja na

1. wadau wa kilimo misitu washirikiane na serikali ili kutekeleza mikakati ya kitaifa na kimataifa hasa mkakati wa kilimo misitu.

2. wadau wote wa kilimo misitu na mazingira kufanya kazi kwa karibu na kamati ya kitaifa ya ushauri ya kilimo misitu.

3. kuanzishwa kwa jukwaa la kilimo misitu lakitaifa litakaloratibu utekelezaji wa mkakati huo pamoja na kuunganisha juhudi na wadau mbalimbali.

4. Wadau wa kilimo misitu wahakikishe kuwa utekelezaji wa mikakati na shughuli zote unachangia moja kwa moja katika kuimarisha usalama wa chakula nchini

Yasinta Nzogera, Mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya mazao kutoka wizara ya kilimo