Mazingira FM
Mazingira FM
14 November 2025, 1:00 pm

Dr. Victor Christopher hospitari ya rufaa ya kumbukumbu ya mwalimu Nyerere inapokea wagonjwa wengi wapya kwa mwezi takribani 2500 hadi 3000.
Na Catherine Msafiri,
Imeelezwa kuwa uzito mkubwa, unywaji wa pombe kupita kiasi, ulaji wa chumvi nyingi vyatajwa kuwa miongoni mwa visababishi vya shinikizo la damu yaani preussure
Hayo yamebainishwa na Dr. Victor Christopher kutoka hospital ya rufaa ya kumbukumbu ya mwalimu Nyerere kitengo cha magonjwa ya ndani alipozungumza kupitia kipindi cha kapu letu wakati wa kutoa elimu ya afya.
Dr. Christopher amebanisha kuwa hakuna dalili za tatizo la shinikizo la damu badala yake madhara yanapotokea ndipo mtu anaweza kugunduliwa kuwa anatatizo hilo kwa kupata kiharusi, upofu wa ghafla, mshituko wa moyo na mapafu kujaa maji
Hatahivyo amebainisha kuwa katika hospitari ya rufaa ya kumbukumbu ya mwalimu Nyerere wanapokea wagonjwa wengi wapya kwa mwezi takribani 2500 hadi 3000.
Kwa upande wake mratibu wa magonjwa yasioambukiza mkoa wa Mara Bi. Ester Muya ameeleza kuwa kila mtanzania anawajibu wa kupima mara kwa mara ili kuwa rahisi kubaini kama anatatizo la shinikizo la damu, kwani ugonjwa huu kwasasa unawapata hata vijana.