Mazingira FM

OCD Butiama: Wananchi achana na propaganda za kulinda kura

27 October 2025, 8:37 pm

Wakili Daudi Mathew Ibrahim  Mrakibu mwandamizi wa polisi na mkuu wa polisi wilaya ya Butiama

Mwenye jukumu la kulinda raia na mali zake kwa mujibu wa ni jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama.

Na Adelinus Banenwa

Wito umetolewa kwa wananchi wilayani Butiama kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 29 oct 2025 kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowataka kwa kuwa usalama umeimalishwa.

Hayo yamesemwa na Wakili Daudi Mathew Ibrahim  Mrakibu mwandamizi wa polisi na mkuu wa polisi wilaya ya Butiama kupitia kipindi cha duru za habari kinachorushwa na Radio Mazingira FM ambapo amesema hadi sasa wilaya ya Butiama ipo shwari na hakuna kiashiria chochote cha uvunjifu wa amani.

Wakili Daudi Mathew Ibrahim  Mrakibu mwandamizi wa polisi na mkuu wa polisi wilaya ya Butiama

Mathew amesema kuwa tangu kipindi cha kampeni kimeanza hadi kuelekea tamati ya kampeni hizo, Jeshi la polisi kupitia elimu iliyokuwa ikitolewa kwa wananchi imesaidia kuongeza uelewa kwa wananchi ndiyo maana amani na utulivu vipo.

Sauti ya Wakili Daudi Mathew Ibrahim  Mrakibu mwandamizi wa polisi na mkuu wa polisi wilaya ya Butiama

Aidha amewataka wananchi kujiepusha na maaneno ya propaganda ambayo yanawataka wananchi kulinda kura akieleza kwamba wananchi hawatakiwi kujihusisha na vitendo hivyo kwa kuwa mwenye jukumu la kulinda raia na mali zake kwa mujibu wa ni jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama hivyo, mwananchi akimaliza kupiga kura anatakiwa kurudi nyumbani na kusubiri matokeo.

Sauti ya Wakili Daudi Mathew Ibrahim  Mrakibu mwandamizi wa polisi na mkuu wa polisi wilaya ya Butiama