Mazingira FM
Mazingira FM
24 October 2025, 1:38 pm

Jumla ya wapigakura wenye sifa kwa mujibu wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ni takribani watu 253.891
Na Adelinu Banenwa
Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Aswenge Enock Kaminyoge amewahakikishia wananchi wilayani Bunda ambao wanasifa za kupiga kura tarehe 29 oct kwenda kutimiza haki yao ya kikatiba kwa kuwa hali ya usalama imeimalishwa.

Akizungumza na viongozi wa dini leo tarehe 23 oct 2025 DC Aswege amesema viongozi wa dini wanayo nafasi ya kwenda kuzungumza na waumini wao juu ya kushiriki uchaguzi mkuu kutokana na umuhimu wake ambao kupitia uchaguzi huo watapatikana viongozi watakaowaletea maendeleo
Ameongeza kuwa katika majimbo matatu ya wilaya ya Bunda jumla ya wapigakura wenye sifa kwa mujibu wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ni takribani watu 253.891 ambapo kati yao jimbo la Bunda Mjini ni 110,674 jimbo la Bunda ELFU 58,907 na jimbo la Mwibara ni 84,310

Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa dini wameishauri serikali kushughulikia changamoto za wananchi ili kupunguza hasira na manung’uniko miongoni kwa changamoto zingine hasa katika huduma za kijamii ikiwemo afya elimu n.k