Mazingira FM

Namba 3 atema cheche akimnadi mgombea CCM

18 October 2025, 8:54 pm

Samwel Kiboye maarufu namba 3 kulia akimnadi mgombea udiwani Bunda stoo katika mkutano wakampeni

Kiboye amesema Chama Cha Mapinduzi kilishafanya maamuzi yake hata kama aliyechaguliwa ulikuwa humpendi ila kwa sasa huyo ndiye aliyeonekana na chama kuwa anafaa.

Na Adelinus Banenwa

Wito umetolewa kwa wanachama wa chama cha mapinduzi kuacha makundi na kuhakikisha wanawapigia wagombea wao kura katika ngazi za udiwani ubunge hadi rais katika uchaguzi mkuu wa tarehe 29 oct 2025.

Hayo yamesemwa na Samwel Kiboye maarufu Namba 3 wakati akimnadi mgombea udiwani kata ya Bunda stoo Flavian Chacha Nyamageko katika mkutano wa kampeni katika eneo la Bigutu leo Oct 17 2025.

Kiboye amesema chama cha mapinduzi kilishafanya maamuzi yake hata kama aliyechaguliwa ulikuwa humpendi ila kwa sasa huyo ndiye aliyeonekana na chama kuwa anafaa akitolea mfano kwamba yeye alishakatwa mara mbili na chama lakini hakuwahi kuchukia wala kutengeneza makundi.

Samwel Kiboye maarufu namba 3 akimsisitiza jambo mhombea udiwani kata ya Bunda stoo Ndug Flavian Chacha

Kiboye amesema kwa mara ya kwanza alikatwa wakati akitetea nafasi yake ya mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara na mara ya pili alikatwa akiwa anatia nia kugombea nafasi ya ubunge jimbo la tarime lakini hakutengeneza chuki wala makundi.

Sauti ya Samwel Kiboye maarufu namba 3
Mgombea udiwani wa kata ya Bunda stoo Flavian Chacha

Kwa upande wake mgombea udiwani wa kata hiyo Flavian Chacha amewaomba wakazi wa Bigutu kata ya Bunda stoo kumchagua ili yale maendeleo aliyoyasimamia katika miaka mitano iliyopita aweze kuyaendeleza.

Amesema katika kata hiyo hakuna mgombea mwingine wa chama kingine cha siasa ila kutokuwepo mpinzani siyo kwamba tayari ameshinda badala yake amewataka wananchi wampigie kura za ndiyo kwa kuwa wakiacha anweza kupigiwa kura za hapana nyingi hivyo akakosa sifa ya kutangazwa

Sauti ya Mgombea udiwani wa kata ya Bunda stoo Flavian Chacha