Mazingira FM
Mazingira FM
16 October 2025, 3:22 pm

Jeshi la polisi limesema limeshajiandaa kikamilifu kusimamia usalama wakati wa uchaguzi kama wanavyofa katika kipindi hiki cha kampeini.
Na Adelinus Banenwa
Jeshi la polisi mkoa wa Mara limewahakikishia wananchi wote mkoani Mara kuwa hali ya usalama ni nzuri na jeshi kinaendelea kushirikiana na wananchi kuimarisha usalama huo.
Hayo yamesemwa na kamanda wa polisi mkoa wa Mara Pius Lutumo alipozunzumza na Radio Mazingira FM kupitia kipindi cha Asubuhi leo ambapo amesema jeshi hilo kupitia program ya polisi jamii angalau kila kata kuna polisi kata mwenye cheo angalau cha mkaguzi msaidizi wa polisi.
Kamanda Lutumo amesema lengo likiwa ni kutoa elimu na kushirikiana na wananchi kudhibiti matukio ya kiharifu kwenye jamii.
Kuelekea uchaguzi mkuu Oct 29 kamanda Lutumo amewahakikishia wananchi hali ya usalama kuwa shwali huku akisisitiza kuwa wao kama jeshi la polisi umeshajiandaa kikamilifu kusimamia usalama kama wanavyofa katika kipindi hiki cha kampeini