Mazingira FM
Mazingira FM
13 October 2025, 11:45 am

Mgombea udiwani kata ya Nyasura Magigi Samwel Kiboko aahidi akichaguliwa malengo yake ni kuhakikisha kinajengwa kituo cha afya chenye hadhi ya hospitali ya wilaya katika kata ya Nyasura.
Na Catherine Msafiri
Mgombea udiwani kata ya Nyasura Magigi Samwel Kiboko ameendelea na kampeni za kuomba kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu katika kata ya Nyasura ambapo ameahidi kuwa kama atachaguliwa ataendeleza maendeleo pale alipoishia.
Ameyasema hayo alipozungumza kwenye mkutano wa hadhara katika mtaa wa Nyasura kata ya Nyasura ambapo ameweka wazi kuwa mpaka sasa tayari anazo fedha kwaajiri ya kujenga shule ya msingi katika kata hiyo hivyo akichaguliwa anakwenda kuanza kazi
Aidha ndugu, Kiboko ameongeza kuwa kama atachaguliwa malengo yake ni kuhakikisha kinajengwa kituo cha afya chenye hadhi ya hospitali .

Akisalimia wakazi wa Nyasura B Diwani viti maalum kupitia chama cha Mapinduzi Seya Locket amewaeleza kuwa viongozi ni wawakilishi wa wananchi katika kutafuta maendeleo hivyo wajitokeze kuwachagua na kuwapa kura kwenye uchaguzi mkuu 29 October 2025
