Mazingira FM
Mazingira FM
9 October 2025, 12:06 pm

Bw.Paul Nesphori mtaalamu wa saikolojia na ujasiri Kutoka hospitali ya rufaa ya kumbukumbu ya mwalimu Nyerere aeleza ukatili wa kijinsia ni chanzo cha matatizo ya afya ya akili katika mkoa wa Mara.
Na Catherine Msafiri,
Ikiwa kesho Dunia ainaadhimisha siku ya Afya ya akili kimataifa ,Imeelezwa kuwa ukatili wa kijinsia unaofanyika kwa wanawake na watoto ni chanzo cha matatizo ya afya ya akili katika mkoa wa Mara.
Hayo yamebainishwa na Bw.Paul Nesphori mtaalamu wa saikolojia na unasihi Kutoka hospitali ya rufaa ya kumbukumbu ya mwalimu Nyerere (Kwangwa) ambapo amebainisha kuwa katika mkoa wa Mara tatizo hilo lipo kwa kiasi kikubwa .
Aidha amebainisha kuwa zipo sababu tofauti tofauti zinazoweza kupelekea mtu akapata tatizo la afya ya akili kama msongo wa mawazo, matumizi ya vilevi na kuna matatizo ya kurithi.
Kwa upande wake Bi.Judithi Vicent afisa habari na mawasiliano ameeleza namna wanavyowafikia wananchi katika kuwapa elimu ya tatizo hilo ili kuweza kupata huduma za kitabibu.
Hata hivyo terehe October 10 kila mwaka Dunia inaadhimisha siku ya afya ya akili lengo likiwa ni kuhamasisha na kutoa elimu kwa jamii kujua umuhimu wa afya ya akili na kuepuka unyanyapaa kwa watu wenye tatizo la afya ya akili.